• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Kenya afanya ziara Afrika Kusini

  (GMT+08:00) 2018-01-12 09:20:09

  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana aliwasili Afrika Kusini kwa ziara ya siku tatu nchini humo, inayolenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

  Serikali ya Kenya ilitoa taarifa kabla ya kuondoka kwa rais Kenyatta ikisema, rais huyo atafanya mazungumzo na mwenzake wa Afrika Kusini Jacob Zuma kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo biashara, usalama na maendeleo ya miundombinu.

  Taarifa pia imesema, kwenye mazungumzo hayo marais hao wawili watajaribu kupitia tena mchakato wa utekelezaji wa makubaliano yaliyosainiwa awali na kutafuta maeneo mapya ya kuimarisha uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako