• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UNHCR lasema wakimbizi laki 1.1 wamerudi Somalia katika miaka mitatu iliyopita

  (GMT+08:00) 2018-01-12 10:18:41

  Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema limewarudisha kwa hiari wakimbizi laki 1.1 wa Somalia kutoka nchi sita tangu mwezi Desemba, mwaka 2014.

  Ofisa wa UNHCR amesema kutokana na takwimu za Desemba wakimbizi elfu 75 wamerudi Somalia kutoka Kenya na elfu 34 kutoka Yemen, na wengine 626 kutoka nchi nyingine kama vile, Djibouti, Eritrea na Tunisia.

  Wataalamu wanasema kuboreka kwa utulivu wa kisiasa na usalama nchini Somalia, pamoja na shinikizo kutoka kwa nchi zilizowapokea wakimbizi hao, vinahimiza kuwepo kwa njia mpya ya kutafuta suluhisho la kudumu kwa wakimbizi kutoka Somalia.

  Shirika hilo limetoa shukurani kwa msaada wa mashirika ya ndege za Kenya na Yemen kuwarudisha wakimbizi hao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako