• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 2,500 wapoteza makazi kutokana na mvua kubwa katikati ya Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-01-12 10:19:09

  Watu zaidi ya 2,500 wamepoteza makazi yao baada ya mvua kubwa kuharibu nyumba 106 katika mji mkuu wa Dodoma nchini Tanzania.

  Mkuu wa wilaya ya Chemba Bw. Simon Odunga amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari, kuwa mvua kubwa ambayo ilianza kunyesha jumanne hadi alhamisi imeathiri vijiji vitatu vya Mrijo Chini, Kaloleni na Olborot.

  Bw. Odunga ameongeza kwamba wengi wa waathirika wamehifadhiwa na jamaa na marafiki, na wengine wanaishi katika kambi maalum, na wanahitaji msaada wa kibinadamu, ikiwa ni pamoja na dawa, magodoro na chakula. Shule tatu zimelazimika kufungwa kutokana na mvua hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako