• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu za Magereza kushindana kesho jumamosi mjini Nairobi

  (GMT+08:00) 2018-01-12 10:25:21

  Jumamosi hii kutafanyika mashindano ya mbio za kutafuta bingwa miongoni mwa timu za askari magereza nchini Kenya katika viwanja vya Uhuru mjini Nairobi.

  Licha ya kushindana kupata bingwa, kwa upande wa wanaume mashindano hayo yatatumika kupata kikosi kitakachoshiriki mashindano ya IAAF ngazi ya taifa ili kutetea ubingwa wake.

  Mwenyekiti wa kamati ya michezo ya Magereza Kenya Benjamin Njoga, amesema kwa kuwa taarifa tayari zilikwishawafikia viongozi wa magereza yote hivyo kama ilivyo desturi, mashindano hayo yatafana.

  Miongoni mwa majina makubwa yatakayoonekana katika mbio hizo zenye urefu tofauti tofauti, ni ya nyota wanaotikisa duniani kwenye riadha Catherine Ndereba, Edith Masai, Susan Sirma, Salina Kosgei and Susan Chepkemei.

  Wengine ni Wilfred Kimitei, Charles Yosei , Mangata Ndiwa, Silas Kiplagat, na Timothy Cheruiyot.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako