• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mchezaji mkongwe zaidi duniani aongeza mkataba wa kucheza klabuni

  (GMT+08:00) 2018-01-12 10:22:12
  Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Japan, Kazuyoshi Miura, ambaye mwezi ujao atatimiza miaka 51 jana alhamisi ameongeza mkataba na timu yake ya Yokohama FC inayoshiriki ligi kuu nchini Japan.

  Mkataba huo mpya unakuwa ni msimu wa 33 kwa nyota huyo tangu aanze kucheza mpira wa miguu na ikiwa ni rekodi ya dunia, huku yeye mwenyewe akidai kuwa anataka kucheza hata atakapofikisha miaka 60.

  Kazuyoshi anakumbukwa zaidi kwa kufungua njia kwa wachezaji wa bara Asia kwenda kucheza ligi za ulaya alipojiunga na Geona ya Itali mwaka 1994 lakini pia akiacha rekodi ya kuifungia magoli 55 timu ya taifa lake aliyoitumikia katika mechi 89.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako