• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UEFA yataja kikosi bora cha mwaka jana Neymar akikosekana

  (GMT+08:00) 2018-01-12 10:22:34
  Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetangaza kikosi chao bora cha mwaka jana ambapo jina la mshambuliaji wa PSG na timu ya taifa ya Brazil Neymar halipo kati majina 11 ya kikosi hicho.

  Mlinda mlango katika kikosi hicho ni Gianluigi Buffon wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia huku beki wa kulia akiwa ni Dani Alves wa PSG na kushoto ni Marcelo wa Real Madrid.

  Walinzi wa kati ni nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos akisaidiwa na Giorgio Chiellini wa Juventus.

  Katika nafasi ya kiungo wapo viungo wawili wa Real Madrid Luka Modric na Toni Kroos huku kiungo wa Manchester City Kelvin De Bruyne ambaye yuko katika kiwango cha juu naye akijumuiyishwa.

  Kwa upande wa ushambuliaji walioingia ni kama kawaida wawili bora zaidi duniani Lionel Messi na Cristiano Ronaldo huku Eden Hazard wa Chelsea naye akitajwa na UEFA katika safu hii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako