• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Thamani ya biashara kati ya China na nchi husika za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" yafikia dola za kimarekani trilioni 1.13

  (GMT+08:00) 2018-01-12 18:33:24

  Takwimu zilizotolewa leo na idara kuu ya forodha ya China zinaonesha kuwa, mwaka jana, thamani ya biashara kati ya China na nchi zilizojiunga na "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ilifikia dola za kimarekani trilioni 1.13.

  Takwimu hizo zinaonesha kuwa, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi za nje kwa mwaka 2017 ilifikia dola za kimarekani yuan trilioni 4.27, ambalo ni ongezeko la asilimia 14.2 ikilinganishwa na mwaka 2016. Kabla ya hapo thamani hiyo ilipungua kwa miaka miwili mfululizo.

  Msemaji wa idara kuu ya forodha ya China Huang Songping amesema, idara hiyo itazidisha ushirikiano wa forodha kati ya China na nchi zilizojiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kuboresha huduma zake ili kuchangia zaidi maendeleo ya uchumi wa ufunguaji mlango.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako