• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uingereza akabiliana na baa kubwa la uchafuzi wa mazingira kwa mpango wa kufuta matumizi ya mifuko ya plastiki

    (GMT+08:00) 2018-01-12 18:37:01

    Waziri Mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May amezindua mkakati mkubwa wa mazingira ambao haijawahi kutokea nchini humo, akiahidi kufuta taka zote za plastiki zinazoweza kuepukika ifikapo mwaka 2042.

    Akizindua Mpango wa Mazingira wa Miaka 25, Bi. May ameeleza mkakati wa serikali wa kuyaacha mazingira katika hali nzuri zaidi ya ilivyokuwa awali. Amesema kuwa serikali yake itafanya kazi na maduka makubwa ili kuyashawishi kutambulisha maeneo yasiyo na mifuko, ambako vyakula havitawekwa kwenye mifuko.

    Waziri mkuu huyo amesema serikali inapanga kuwekeza fedha kwenye ubunifu wa plastiki kupitia mpango wa utafiti na maendeleo ambao utatengewa dola za kimarekani bilioni 9.5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako