• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tullow yatenga dola milioni 170 kwa maandalizi ya usafirishaji mafuta

  (GMT+08:00) 2018-01-12 18:56:50

  Kampuni ya uchimbaji mafuta ya Tullow Oil imetenga dola milioni 170 kwa shughuli zake nchini Kenya mwaka huu. Kampuni hiyo imesema fedha hizo zitatumiwa kwa uchimbaji na maandalizi ya usafirishaji wa mafuta yaliyopatikana Turkana. Aidha kampuni hiyo imesema ratiba yake ilitatizwa na kipindi kirefu cha uchaguzi mwaka uliopita hivyo basi imeshauriana upya na serikali kabla ya mafuta yaanze kusafirishwa kutoka Turkana hadi Mombasa. Shughuli za uchimbaji katika eneo la Lokichar Kusini, kaunti ya Turkana zilikamilika na sasa kazi zinazoendelezwa ni zinazolenga kutoa mafuta ardhini.Tullow inanuia kutangaza utathmini wake kuhusu kiwango kamili cha mafuta yaliyopatikana pamoja na hatua zitakazopigwa itakapotoa ripoti ya kina Februari 17.Usafirishaji wa mafuta hayo kwa barabara utakuwa wa kujaribu kama Kenya itafaidika kutokana na biashara hiyo kabla bomba la kusafirisha mafuta lijengwe kutoka Turkana hadi Mombasa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako