• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yawataka wakuu wa mikoa kusimamia uuzaji wa mbolea kwa wakulima

    (GMT+08:00) 2018-01-12 18:57:12
    Waziri wa Kilimo wa Tanzania Bw Charles Tizeba amewaagiza wakuu wa mikoa, kusimamia usambazaji wa mbolea zinazoingia katika mikoa yao ili kuhakikisha zinawafikia wakulima vijijini kwa bei iliyopangwa na serikali.

    Akizungumza na na waandishi wa habari, Bw Tizeba amewataka wafanyabiashara wasimamiwe ili wasiuze kinyume na bei elekezi, lakini pia hakuna sababu ya kuwaumiza wasafirishaji wakubwa kwa sababu na wao wanahitaji kupata faida.

    Mapema mwaka jana, serikali kupitia iliyokuwa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ilitangaza utaratibu wa kuagiza mbolea kwa pamoja na kuweka bei elekezi katika mbolea za kupandia na kukuzia, ambapo mbolea ya DAP haitakiwi kuuzwa zaidi ya shilingi 56,000 na UREA isizidi shilingi 48,000.

    Aidha, bei hiyo elekezi inatofautiana na maeneo kulingana na umbali kutoka jijini Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako