• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utalii umekuwa motisha ya ongezeko la uchumi duniani

    (GMT+08:00) 2018-01-12 19:22:13

    Waraka wa utalii unaohusu uchambuzi na makadirio kuhusu maendeleo ya utalii nchini China ya mwaka 2016-2017 umetolewa leo hapa Beijing.

    Waraka huo wenye kauli mbiu ya "mageuzi na uvumbuzi wa sekta ya utalii ya China katika zana mpya", umetoa makadirio kuhusu maendeleo ya utalii ya China katika mwaka 2017-2018, na kuchambua masuala nyeti ya maendeleo ya utalii duniani.

    Wakara huo unasema, mwaka 2017 hali ya uchumi katika nchi kubwa duniani imeboreshwa, imani ya watu wa nchi mbalimbali kuhusu uwezo wao wa kiuchumi imeinuka, mahitaji ya utalii katika nchi hizo yameongezeka hatua kwa hatua, miundo mbinu ya utalii unaovuka mipaka imeboreshwa, gharama za utalii umepungua, na njia ya kupata viza imekuwa rahisi zaidi. Kutokana na hali hiyo, idadi ya jumla ya watalii na mapato ya jumla ya utalii duniani umedumisha mwelekeo wa ongezeko kubwa, na utalii umekuwa motisha muhimu kwa ongezeko la uchumi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako