• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UN asifu kundi la nchi 77 na China

    (GMT+08:00) 2018-01-13 17:07:59

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesifu sana umuhimu ulioonyeshwa na kundi la nchi 77 na China katika kulinda ushirikiano wa pande nyingi, kuhimiza maendeleo na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Alisema hayo kwenye sherehe ya kukabidhiwa kwa unyekiti wa kundi la nchi 77 kutoka Ecuador kwenda Misri, ambayo ilifanyika jana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

    Bw. Guterres amesema, kundi la nchi 77 na China ni nguvu kuu ya kulinda ushirikiano wa pande nyingi, na zimetoa mchango mkubwa katika kuhakikisha Umoja wa Mataifa unachukulia maendeleo kuwa kazi yake kuu. Vilevile amesifu India na China ambazo ni nchi kubwa mbili kiuchumi kwenye kundi la nchi 77, kwa juhudi zao za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako