• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kulinda nafasi ya kiini ya rais Xi ni muhimu

    (GMT+08:00) 2018-01-13 17:23:30

    Jambo la muhimu katika kutekeleza mtazamo wa mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC ni kulinda nafasi ya kiini ya rais Xi Jinping katika Kamati Kuu ya CPC na Chama kizima na pia kulinda mamlaka ya Kamati Kuu ya CPC na uongozi wake mkuu.

    Hayo yamo kwenye taarifa iliyopitishwa katika kikao cha 2 cha wajumbe wote cha Kamati Kuu ya 19 ya Kusimamia Nidhamu CCDI ya CPC, ambacho kilifanyika kuanzia Alhamisi hadi Jumamosi wiki hii.

    Kitu kingine muhimu ni kujifunza na kushikilia Fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye Umaalumu wa Kichina katika Kipindi Kipya na kuifanya iongoze vitendo na kazi.

    CCDI pia imesisitiza juhudi za kutekeleza kithabiti usimamizi kamili na mkali kwa Chama.

    Taarifa hiyo imesema hivi sasa vita dhidi ya ufisadi bado ni muhimu na ina utata, na usimamizi kamili na mkali kwa Chama haupaswi kuishia njiani, na ni lazima kuwe nia na uvumilivu katika kufanya vita hiyo ambayo haitasimama kamwe dhidi ya ufisadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako