• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasema kauli ya Rais Trump dhidi ya wahamiaji kutoka Haiti na Afrika ni ya kutia aibu na ya kibaguzi

    (GMT+08:00) 2018-01-13 18:23:50

    Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa UNHCR imetafsiri kauli ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu wahamiaji kutoka nchi kama Haiti na Afrika kuwa "ya kushtua, kutia aibu na kibaguzi.

    Habari zinasema Rais Trump Alhamisi alikejeli kwa lugha ya matusi kwenye mkutano na kuuliza kwa nini Marekani inapokea wahamiaji wengi kutoka Haiti na Afrika, wala sio maeneo mengine kama Norway.

    Katika hatua nyingine naibu katibu mkuu wa chama tawala cha ANC cha Afrika Kusini Jessie Duarte amemkera vikali Rais Trump, akimlaumu kutokana na kauli zilizojaa matusi na dharau dhidi ya nchi zinazoendelea husuani Afrika.

    Naye waziri wa mambo ya nje wa Cuba, amemshutumu vikali Rais Trump na kusema kuwa maneno yake yamejaa ubaguzi, kuzipaka matope na yasiyokuwa na adabu dhidi ya nchi za Haiti, El Salvador pamoja na Afrika.

    Lakini Rais Trump alikanusha kutoa lugha ya matusi baada ya kulaumiwa na jumuiya ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako