• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kuthamini makubaliano ya nyuklia ya Iran

    (GMT+08:00) 2018-01-14 18:20:01

    China imezitaka pande mbalimbali kuthamini makubaliano ya nyuklia ya Iran baada ya Marekani kuamua kuongeza muda wa kusitisha vikwazo dhidi ya Iran.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Lu Kang ametoa kauli hiyo akitoa maoni kuhusu taarifa hiyo ya Marekani. Amesema China imefuatilia taarifa ya Marekani na pia imegundua kuwa jumuiya ya kimataifa inaunga mkono makubaliano hayo, na kupongeza Iran kwa kuyatekeleza kikamilifu. Ameongeza kuwa pande mbalimbali zinatakiwa kudhibiti mwafaka migongano yao na kuendelea kutekeleza kikamilifu makubaliano hayo.

    Siku hiyo waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alizungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif, na kubadilishana naye juu ya taarifa mpya ya Marekani kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Iran. Bw. Wang Yi amesisitiza kuwa China itadumisha mawasiliano na pande mbalimbali ikiwemo Iran na kufanya kazi za kiujenzi katika kulinda na kutekeleza ipasavyo makubaliano hayo muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako