• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Mashindano ya CHAN: Uganda yaanza vibaya, na Rwanda kucheza leo

    (GMT+08:00) 2018-01-15 10:22:52

    Kwenye siku ya pili tangu kuanza kwa michuano ya kombe la mataifa kwa wachezaji wa ndani (CHAN) nchini Morocco, Timu za Sudan, Namibia, na Zambia zimefanikiwa kupata ushindi.

    Sudan iliishinda Guinea ya Conakry kwa magoli 2-1 katika mechi ya pili ya kundi A iliyofanyika mjini Casablanca, na kwa upande wa kundi B, Namibia iliifunga Ivory Coast kwa goli 1-0.

    Lakini katika mechi ya pili ya kundi hilo matekoe hayakuwa mazuri kwa vinara wa Afrika mashariki kwa sasa Uganda, kwani walifungwa na Zambia kwa magoli 3-1 kwenye uwanja wa Marrakech.

    Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi mbili zitakazopigwa mjini Tangier ambapo wawakilishi wengine wa Afrika Mashariki, timu ya taifa ya Rwanda watashuka dimbani kucheza na Nigeria.

    Na mechi ya pili itakuwa baina ya mabingwa wa michuano hiyo wa mwaka 2014, Libya amabao watacheza dhidi ya Equatorial Guinea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako