• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikapu, Ligi kuu Uganda: City Oil yatetea ubingwa wake

    (GMT+08:00) 2018-01-15 10:23:12

    Nako nchini Uganda, timu ya City Oilers imefanikiwa kutetea ubingwa wake katika ligi kuu ya mpira wa kikapu baada ya kuifunga timu ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) kwa alama 68-60 kwenye mechi ya nne ya fainali kuu.

    Hata hivyo ushindi huo, ulikuwa ni wa nne katika mfululizo wa mechi saba za fainali ilizocheza dhidi ya KIU.

    Oilers wanashinda taji hilo kwa mara ya tano mfululizo, na kuvunja rekodi ya kwao wenyewe ya kushinda mara nne waliyoweka msimu uliopita.

    Landry Ndikumana wa City Oilers alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi za fainali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako