• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpira wa Magongo, Kenya: Timu ya Telkom yashinda ubingwa wa ligi kuu ya wanawake

    (GMT+08:00) 2018-01-15 10:23:50
    Timu ya Telkom imefanikiwa kutetea taji lake la ligi kuu ya mpira wa magongo kwa upande wa wanawake ya nchini Kenya ikiwa bado ina mechi mbili za kucheza msimu huu.

    Telkom jana iliishinda timu ya Chuo Kikuu cha Multimedia (MMU) kwa magoli 6-0 na kuifanya ifikishe alama 54 kwenye msimamo ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote.

    Mabingwa hao watetezi sasa wanatwaa taji hilo kwa mara ya ishirini na wakiwa na rekodi ya kushinda mechi zote 18 walizokwisha cheza msimu huu, wakifunga jumla ya magoli 109 na wakiruhusu nyavu zao kufungwa mara tatu tu.

    Kocha mkuu wa timu hiyo Jos Openda amewapongeza wachezaji wake, na amesema sasa kwa kuwa upande wa ligi kazi imekwisha, sasa nguvu zao wanazielekeza kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika jumamosi ijayo mjini Accra nchini Ghana.

    Timu zinzgine zinazoshiriki mashindano hayo ya Afrika ni Strathmore ya Kenya, KADA Queens na Yobe Desert Queens za Nigeria pamoja GRA na Polisi zote za Ghana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako