• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Michael Olunga afunga hatrick nchini Hispania

    (GMT+08:00) 2018-01-15 10:24:07
    Mshambuliaji wa klabu ya Girona nchini Uhispania, Mkenya Michael Olunga ameweka historia siku ya Jumamosi iliyopita, na kuwa mchezaji wa kwanza wa Kenya kufunga hatrick (magoli matatu kwenye mechi moja) katika ligi ya Uhispania huku wakiishinda klabu ya Las Palmas 6-0.

    Olunga aliingia kama mchezaji wa ziada na kufunga katika dakika ya 57, 70 na 79 na kuwa mshambuliaji wa kwanza wa klabu ya Girona kufunga hat-rick katika msimu wake wa kwanza katika ligi ya La Liga.

    Ushindi huo ulikuwa mkubwa kwa klabu hiyo ya Catalan tangu iingie katika ligi ya La Liga.

    Olunga mwenye umri wa miaka 23 anaichezea Girona kwa mkopo kutoka klabu ya China ya Guizhou Hengfeng.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako