• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ligi Kuu ya Uingereza. Hatimaye rekodi ya Manchester City yakutofungwa yafutwa

    (GMT+08:00) 2018-01-15 10:24:30
    Rekodi ya Manchester City ya kutofungwa katika mechi arobaini tangu mwezi April mwaka jana imekatizwa jana kufuatia kipigo cha magoli 4-3 na Liverpool katika uwanja wa Anfield.

    Magoli ya Liverpool kwenye mechi hiyo yalifungwa na Alex Oxlade Chamberlain, Roberto Firmino, Sadio Mane na Mohamed Salah, huku magoli ya kufutia machozi kwa upande wa City yakifungwa na Bernardo Silva, Ilkay Gundogan na Sergio Aguero.

    Kwa ushindi huo Liverpool wanaendeleza rekodi ya kutokubali kufungwa na Man City katika uwanja wao wa nyumbani, na sasa wamefanikiwa kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

    Na katika mechi nyingine iliyopigwa jana, Arsenal imefungwa na AFC Bournemouth kwa magoli 2-1 katika uwanja wa Vitality.

    Yote haya yanatokea wakati huu ambapo habari zimetapakaa kuwa, nyota wa timu hiyo Alexis Sanchez akiwa mbioni kuondoka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako