• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kasi ya ongezeko la biashara ya China na nje yaweka rekodi mpya mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-01-15 18:10:17

    Takwimu zilizotolewa na idara ya biashara ya nje iliyo chini ya Wizara ya Biashara ya China zimeonesha kuwa, thamani ya jumla ya uuzaji na uagizaji bidhaa nje ya China kwa mwaka jana ilifikia dola za kimarekani trilioni 4.3, na kutimiza ongezeko la asilimia 14.2, kasi ambayo ni ya juu zaidi katika miaka sita iliyopita.

    Mkurugenzi wa idara ya biashara ya nje katika Wizara ya Biashara ya China Ren Hongwu amesema, kasi hiyo kubwa imetokana na kufufuka kwa soko la kimataifa, kuboreka kwa uchumi wa China, ufanisi wa sera zilizotolewa na serikali ya China, kuongezeka kwa kasi ya marekebisho ya muundo wa kampuni na mabadiliko ya injini zao, na pia biashara ya China na nje kuwa ndogo kiasi katika miaka kadhaa iliyopita.

    Hata hivyo, Bw. Ren amesema anatarajia kuwa mwaka huu biashara ya China na nje itaendelea kuongezeka, lakini huenda kwa kasi ya chini. Amesema kuwa vitendo vya kujilinda kibiashara katika baadhi ya nchi vitaweza kuathiri maendeleo mazuri ya uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako