• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: maduka 95 ya kubadilisha na kununua fedha za kigeni yamefungwa baada ya sheria mpya

    (GMT+08:00) 2018-01-15 20:18:19

    Waendeshaji angalau 95 wa maduka ya kubadilisha na kununua fedha za kigeni nchini Tanzania zimefungwa katika miezi sita iliyopita baada ya kushindwa kufikia mahitaji ya leseni mpya ya uendeshaji shughuli.

    Mnamo Juni mwaka jana, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilipatia maduka hayo, hadi Desemba 31, 2017 kuomba leseni mpya za biashara chini ya mipango mapya.

    Chini ya mpango mpya, mtu hataruhusiwa kufungu zaidi ya duka moja, na angalau theluthi mbili ya mtaji unaotakiwa lazima iwe katika mfumo wa pesa taslimu.

    Hatimaye, maduka hayo, yanahitajika kuunganishwa na kamera za CCTV.

    Uamuzi wa kurekebisha hali ya utoaji leseni kwa maduka ya kubadilisha pesa ni kama njia moja ya kuhakikisha kwamba ofisi hizo hazitumiwi kwa madawa ya kulevya na fedha haramu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako