• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China imekuwa kitovu cha minyororo ya ugavi wa bidhaa duniani

    (GMT+08:00) 2018-01-16 10:06:55

    Naibu mkurugenzi wa kwanza wa shirika la Fedha la kimataifa IMF Bw. David Lipton amesema, China imekuwa mwenzi muhimu wa kibiashara wa zaidi ya nchi 100 duniani, na imekuwa kitovu cha minyororo ya ugavi wa bidhaa duniani.

    Amesema China peke yake inachangia theluthi moja ya ukuaji wa uchumi duniani, na inaongoza nchi nyingine katika sekta za biashara ya digitali, teknolojia ya kifedha, na akili bandia.

    Pia ameeleza kuwa wawekezaji wa China wanaendelea kutoa mchango muhimu katika maendeleo ya sekta ya miundombinu, wakati huo huo uwekezaji wake wa moja kwa moja katika nchi za nje pia umeongezeka siku hadi siku, na kuzinufaisha nchi nyingine zinazoendelea duniani.

    Ameongeza kuwa shirika hilo linathamini sana mchango wa China, na kutarajia ushirikiano utaimarishwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako