Licha ya umahiri wa Nigeria wa kumiliki mechi hiyo, vijana wa Amavubi wakiongozwa na Djihad Bizimana (aliyetangazwa mchezaji bora wa mechi) walimudu kuwianisha umiliki wa mpira kati ya pambe mbili hizo.
Baada ya kuanza vizuri mechi hiyo, Rwanda sasa ili waweze kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele watalazimika kupata matokeo mazuri katika mechi ijayo watakapocheza na Equatorial Guinea siku ya alhamisi mjini Tangier.
Katika mechi nyingine ya kundi C iliyopigwa jana Libya walishinda kwa magoli 2-0 dhidi Equatorial Guinea.
Na michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi mbili za kundi D zitakazopigwa mjini Agadir, ambako Angola watacheza na Burkina Faso, huku Cameroun dhidi ya Congo-Brazzaville.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |