• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja uliongezeka kwa asilimia 7.9 mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-01-16 16:37:56

    Wizara ya Biashara ya China imesema uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja China bara kwa mwaka jana uliongezeka kwa asilimia 7.9 na kufikia dola za kimarekani bilioni 136.33.

    Uwekezaji wa moja kwa moja usiohusu mambo ya kifedha uliofanywa na wawekezaji wa ndani ya China katika nchi na sehemu 173 duniani ulipungua kwa asilimia 30 na kufikia dola za kimarekani bilioni 120.

    Chansela wa biashara wa idara ya ushirikiano katika Wizara ya Biashara ya China Han Yong amesema, kinachostahili kufuatiliwa zaidi ni kuwa mwaka jana fedha zilizokusanywa na makampuni ya China nje ya nchi katika kuwekeza na kununua makampuni ya kigeni zilifikia dola za kimarekani bilioni 75, na kuchukua asilimia 80 ya thamani ya jumla ya fedha zinazohitajika katika shughuli hizo, jambo linaloonesha kuwa uwezo wa makampuni ya China katika kukusanya fedha umeongezeka.

    Wakati huohuo, uwekezaji wa kigeni ulioingia kwenye sekta ya teknolojia ya juu uliongezeka kwa asilimia 14.5 na makampuni ya kigeni yasiyochukua asilimia zaidi ya 3 ya makampuni yote nchini China yamechangia nusu ya thamani ya uuzaji bidhaa nje ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako