• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Volkswagen kutangaza mpangowa kuwekeza Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-01-16 20:48:15

    Kampuni ya ujerumani ya kutengeneza magari Volkswagen inatarajiwa wiki hii kutangaza mpango wake wa kufungua kiwanda nchini Rwanda.

    Mwenyekiti wa kampuni hiyo kanda ya kusini wa Afrika Thomas Schäfer, anatarajiwa Kigali ambapo atafanya mikutano kadhaa na wadau husika kabla ya kuandaa kikao na wana habari baadaye alhamis.

    Baadhi ya mipango inayotarajiwa ni tarehe kamili ya kufungua kiwanda hicho, nafasi za ajira kiasi cha fedha kitakachowekezwa.

    Kulingana na mkataba wa awali wa maelewano kati ya Volkswagen na serikali ya Rwanda, kampuni hiyo itaanza kwa kuzalisha magari 2,000 kwa mwaka.

    Inalenga soko la Rwanda na pia nchi jirani .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako