• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania na Rwanda kujenga reli ya kisasa

    (GMT+08:00) 2018-01-16 20:50:16

    Ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda umezidi kushika kasi, kuelekea kutanua wigo wa ukuaji sekta za biashara na ajira, baada ya juzi marais John Magufuli wa Tanzania na Paul Kagame wa Rwanda, kukubaliana kuanza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ndani ya mwaka huu, iweze kuziunganisha nchi hizo haraka zaidi.

    Ujenzi wa reli hiyo ya kisasa, mbali ya kuongeza kasi ya biashara baina ya nchi hizo mbili, kati ya sita zilizomo Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), itazinufaisha pia nchi nyingine za EAC, Burundi, Uganda na jirani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambayo si mwanachama wa jumuiya ya EAC.

    Nchi nyingine zilizomo katika jumuiya ya Afrika Mashariki ni Kenya na Sudan Kusini.

    Tayari Rwanda na Tanzania zinaunganishwa kwa uhakika kwa njia ya barabara ya lami na kwa anga kutoka Jijini Dar es Salaam.

    Aprili mwaka jana, marais hao walizindua rasmi Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma ya Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako