• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Utegemezi wa bajeti wapungua kwa asilimia mbili ya Pato la Taifa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-01-16 20:50:16

    Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaonyesha kuwa mkakati ya Serikali kusimamia ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi yake umepunguza kiasi cha utegemezi wa bajeti kwa asilimia mbili ya Pato la Taifa.

    Ripoti hiyo ya mwaka wa fedha 2016/17 iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita inaonyesha utegemezi huo umepungua kutoka asilimia 3.5 ya Pato la Taifa mwaka 2015/16 mpaka asilimia 1.5.

    Ripoti inabainisha baadhi ya mambo yalichangia hilo kuwa ni mwenendo mzuri wa ukuaji uchumi kwa asilimia 7.0 mwaka 2016, kuendelea kushuka mfumuko wa bei na ongezeko la makusanyo ya mapato kulifanikiwa kupunguza utegemezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako