• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la WFP lasema msaada wa dharura wa chakula unahitajika Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-01-17 09:26:23

    Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema hali ya usalama ya chakula nchini Sudan Kusini itakuwa mbaya zaidi kwa mwaka huu, kama mamilioni ya watu hawatapatiwa msaada wa dharura wa chakula kabla ya msimu wa masika.

    Naibu mkuu wa WFP Bw Simon Cammelbeek amesema shirika hilo linahitaji kusambaza chakula haraka kwa kwa ajili ya watu milioni sita walioko kwenye maeneo yasiyofikika kirahisi kabla ya msimu wa masika. Ameongeza kuwa kwa sasa hali ya usalama ya chakula si nzuri, kiasi cha mavuno kwa mwaka jana kilipungua ikilinganishwa na miaka iliyopita.

    Ripoti iliyotolewa mwaka jana na Shirika la usalama wa chakula duniani IPC imesema hali mbaya kwenye msimu wenye mavuno machache itawafanya watu milioni 5.1, sawa na asilimia 48 ya wananchi wa Sudan Kusini kukumbwa na msukosuko wa chakula kuanzia mwezi Januari hadi Machi mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako