• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kriketi, Timu ya Kenya itacheza leo na New Zealand

    (GMT+08:00) 2018-01-17 11:19:25
    Kwingineko Timu ya Taifa ya Kenya ya mchezo wa Kriketi, leo inatarajiwa kucheza na wenyeji wa mashindano ya kombe la dunia kwa vijana chini ya miaka 19, New Zealand mjini Christchurch.

    Hii ni mechi ya pili kwa Kenya ambao ni mabingwa wa Afrika, baada ya kucheza mechi ya kwanza jumapili iliyopita ambayo walifungwa na Afrika Kusini.

    Kuelekea mechi ya Leo, kocha mkuu wa timu hiyo Jimmy Kamande, amesema tayari amefanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika mechi iliyopita, hivyo akitarajia matokeo mazuri katika mechi ya leo.

    Kenya iko kundi A la mashindano hayo pamoja na timu za Afrika Kusini, New Zealand na mabingwa watetezi wa michuano hiyo West Indies.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako