Akizungumza baada ya hafla ya utiaji saini kwenye makao makuu ya klabu hiyo mjini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniphace Mkwasa amesema mkataba huo utakuwa na ongezeko kutokana na makubaliano waliyofikia na dau litakuwa likiongezeka kulinganana idadi ya mauzo ya jezi za mashabiki.
Mkataba huu unakuja ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kampuni ya Macron kusaini mkataba wa miaka miwili na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya udhamini wa jezi za timu zote za taifa za soka nchini Tanzania.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |