• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Tetesi za Usajili: Mkhitaryan akwamisha amkwamisha Sanchez kwenda Manchester United, Lakini Walcot atajiunga na Everton.

    (GMT+08:00) 2018-01-17 11:20:28
    Suala la usajili wa Alexis Sanchez wa kujiunga na Manchester United jana limeingia katika sura mpya baada ya kusemekana kuwa Arsenal wanamtaka Henrikh Mkhitaryan wa United atumike kama sehemu ya usajili wa Alexis Sanchez.

    Wakala wa Mkhitaryan, Mino Raiola amesema dili hilo limefikia ugumu sasa baada ya Mkhitaryan mwenyewe kutokuwa tayari kwenda Arsenal na hajazungumza chochote kuhusu hilo.

    Na katika hatua nyingine, Nyota wa Arsenal, Theo Walcot jana amefanyiwa vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na Everton.

    Habari zinasema kuwa Walcot atajiunga na Everton kwa ada ya uhamisho kiasi ya pauni milioni 20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako