• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa asifu hatua za China za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2018-01-17 18:25:59

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesifu hatua muhimu zinazochukuliwa na China katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuhamasisha China kuendelea kutekeleza wajibu wake muhimu katika siku zijazo.

    Bw. Guterres amesema hayo alipokutana na waandishi wa habari, na kuongeza kuwa, hakuna uhakika kuwa ahadi zote zilizotolewa na Mkataba wa Paris zitatimizwa, wala hazitaweza kudhibiti ongezeko la joto duniani chini ya nyuzi mbili kwenye kipimo cha Selisiasi. Pia amesema ushindi bado haujapatikana katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Lakini amesema ana imani kubwa kwa mazungumzo na ushirikiano na serikali ya China katika kukabiliana na mabadiliko hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako