• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AIIB ni benki ya maendeleo ya pande mbalimbali inayoendeshwa kwa vigezo vya kimataifa

    (GMT+08:00) 2018-01-17 19:00:26

    Mwenyekiti wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB Bw. Jin Liqun amesema, benki hiyo siyo benki ya China, bali ni benki ya maendeleo ya pande mbalimbali inayoendeshwa kwa vigezo vya kimataifa.

    Bw. Jin amesema, AIIB ni benki iliyoanzishwa kutokana na pendekezo la China, huku akiongeza kuwa benki hiyo ilizinduliwa kupitia mazungumzo ya nchi wanachama 57 waliotoa mitaji na sasa ina nchi wanachama 84, na ni benki ya maendeleo inayoendeshwa kwa vigezo vya kimataifa na usimamizi wa karne 21.

    Jin amesema hayo kwenye mazungumzo kuhusu ushawishi wa sera za China kwa maendeleo ya kiuchumi ya kimataifa kwenye kongamano la fedha la Asia lililomalizika jana. Amesema, lengo la China kupendekeza benki hiyo ni kuzidisha juhudi za mashirika yanayokuwepo kama Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Asia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako