Uganda ambayo iko kundi B, leo itahitaji ushindi itakapocheza dhidi ya Namibia ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali, kwa kuwa tayari ilikwisha poteza kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Zambia.
Mechi nyingine ya Kundi B, itazikutanisha Ivory Coast na Zambia, lakini katika kipekee kutoka kundi A la mashindano hayo, Morocco na Sudan zimefuzu hatua ya robo fainali baada ya ushindi zilioupata katika mechi za pili za hatua ya makundi.
Morocco ilishinda kwa magoli 3-1 dhidi ya Guinea ya Conakry, Sudan ikishinda kwa goli 1-0 dhidi ya Mauritania.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |