• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gofu, Zawadi ya bingwa wa mashindano ya Kimataifa ya Kenya yaongezwa

    (GMT+08:00) 2018-01-18 08:14:39
    Zawadi ya bingwa wa mwaka huu katika mashindano ya kimataifa ya mchezo wa gofu nchini Kenya (maarufu kama Kenya Open), imeongezwa kwa asilimia 127 kutoka ile ya zamani.

    Katika mshindano hayo yatakayofanyika kuanzia machi 22 hadi 25 bingwa atazawadiwa Euro 500,000 ambayo ni sawa na shilingi milioni 69 za Kenya tofauti na zawadi ya miaka ya nyuma ya Euro 220,000.

    Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya maandalizi, Peter Kanyago, takribani wachezaji 150 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo yatakayofanyika katika uwanja wa klabu ya gofu ya Muthaiga mjini Nairobi.

    Mwenyekiti huyo amesema, licha ya kuwa kujitokeza kwa wingi kwa wadhamini ndiko kulikochangia nyongeza ya zawadi, pia changamoto iliyotolewa na Rais Uhuru Kenyatta alipokuwa mgeni rasmi katika mashindano yaliyopita kumechangia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako