Katika tuzo hiyo kwa mwaka huu Caster anashindana na nyota wengine duniani wakiwemo, wachezaji wa tennis Serena Williams wa Marekani, Garbine Muguruza wa Hispania, bingwa wa michezo ya kuteleza kwenye barafu Mikaela Shriffin wa Marekani na Chipukizi nyota katika mchezo wa kuogelea kutoka Marekani.
Akitoa pongezi za serikali, Rais wa chama cha riadha cha Afrika Kusini, Alech Skhosana, pamoja na mambo mengine, amesema taifa zima lina imani na Caster, vile vile linaamini atatwaa tuzo hiyo, huku akimshukuru kocha wa mwanamichezo huyo ambaye ni bingwa mara tatu wa mbio za mita 800 wanawake duniani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |