• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Timu za Morocco na Sudan zafuzu rodo fainali ya CHAN

  (GMT+08:00) 2018-01-18 08:47:18

  Timu ya taifa ya Uganda ishuka uwanjani leo kucheza na Namibia katika mechi yake ya pili ya hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani.

  Uganda ambayo iko kundi B, leo itahitaji ushindi itakapocheza dhidi ya Namibia ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali, kwa kuwa tayari ilikwisha poteza kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Zambia.

  Mechi nyingine ya Kundi B, itazikutanisha Ivory Coast na Zambia, lakini katika kipekee kutoka kundi A la mashindano hayo, Morocco na Sudan zimefuzu hatua ya robo fainali baada ya ushindi zilioupata katika mechi za pili za hatua ya makundi.

  Morocco ilishinda kwa magoli 3-1 dhidi ya Guinea ya Conakry, Sudan ikishinda kwa goli 1-0 dhidi ya Mauritania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako