• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya umoja wa mataifa yahitaji dola bilioni 1.6 kuwafikia wasomali milioni 5.4 wenye mahitaji

    (GMT+08:00) 2018-01-18 08:56:43

    Mashirika ya umoja wa mataifa yanayofanya kazi nchini Somalia, yamezindua mwito wa kupatiwa dola bilioni 1.6 za kimarekani, kwa ajili ya kutoa misaada ya kibinadamu ya kuokoa maisha, kwa wasomali milioni 5.4 wanaohitaji msaada kwa mwaka huu.

    Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Somalia Bw Peter de Clercq, jana mjini Mogadishu alizindua mpango wa mwitikio wa kibinadamu kwa mwaka huu, na kusema fedha hizo zinahitajika ili kuokoa maisha ya watu milioni 5.4 walioathiriwa na ukame mkali. Amesema mwaka jana kutokana na ushirikiano na serikali ya Somalia na jumuiya ya kimataifa, walifanikiwa kuepusha njaa.

    Hata hivyo amesema suluhisho la kudumu kwa matatizo ya ukame, mgogoro na watu kukimbia makazi yao bado liko mbali, kwa hiyo kazi nyingi zinatakiwa kufanywa ili kuondoa njaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako