• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM asisitiza kulinda makubaliano ya nyuklia ya Iran

    (GMT+08:00) 2018-01-18 09:33:49

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres ametoa taarifa kupitia msemaji wake akisisitiza kulinda makubaliano ya nyuklia ya Iran.

    Taarifa hiyo imesema Bw. Guterres anaamini kuwa makubaliano hayo ni njia nzuri ya kuhakikisha kuwa mpango wa nyuklia wa Iran ni kwa ajili ya matumizi ya amani, na ni mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye kazi ya kutoeneza silaha za nyuklia na sekta ya diplomasia, na kutoa mchango kwa amani na usalama wa kikanda na kimataifa.

    Anaona shirika la kimataifa la nishati ya Atomiki IAEA limethibitisha mara nyingi kuwa Iran inatekeleza ahadi zinazohusiana na suala la nyuklia.

    Taarifa pia imesema Bw. Guterres alisisitiza kuwa ufuatiliaji wowote kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia ya Iran unapaswa kutatuliwa kupitia utaratibu uliowekwa kwenye makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako