• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yaahidi msaada wa kupambana na homa ya Chikungunya katika pwani ya Kenya

    (GMT+08:00) 2018-01-18 09:49:00

    Shirika la afya duniani WHO imeahidi kushirikiana na Wizara ya afya ya Kenya kusaidia kupambana na homa ya Chikungunya inayoambukizwa na mbu mjini Mombasa. WHO imesema Wizara ya afya na serikali ya kaunti ya Mombasa zitaimarisha udhibiti, utambuzi na matibabu ya maambukizi mapya ya ugonjwa huo.

    Mwakilishi wa WHO nchini Kenya Bw. Rudi Eggers amesisitiza kuwa timu ya ufundi ya WHO iko tayari kuisaidia serikali ya Kaunti ya Mombasa kupambana kwa ufanisi na ugonjwa huo baada ya kuenea kwa kiasi kikubwa.

    Wizara ya Afya ya Kenya Januari 4 iliripoti maambukizi 69 ya Chikungunya mjini Mombasa, na kuahidi kuyasimamia na kutoa matibabu kwa wakati ili kuzuia kuenea kwake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako