• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China amaliza ziara yake barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-01-18 09:50:58

    Waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi amesema, China na nchi za Afrika zitakuwa wenzi wa karibu zaidi kutokana na ushirikiano wa Pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja".

    Bw Wang amesema hayo alipohitimisha ziara yake ya kwanza kwa mwaka iliyomfikisha Rwanda, Angola, Gabon na Sao Tome na Principe.

    Bw. Wang Yi amesema Afrika siku zote ni kituo cha kwanza kwa ziara ya waziri wa mambo ya nje ya China katika miaka 28 iliyopita. Amesema hii ni desturi nzuri inayoonyesha jumuiya ya kimataifa kwamba China daima inasimama pamoja na ndugu zake wa Afrika.

    Pia amesema China itatafuta ushirikiano na Afrika kujenga uaminifu na ushirikiano wa dhati, bila kujali itakuwa na maendeleo kiasi gani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako