• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe awataka Wazimbabwe walio nje ya nchi kuwekeza nyumbani

    (GMT+08:00) 2018-01-18 16:20:30

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amewaalika wafanyabiashara wa Zimbabwe walioko nchini Msumbiji kurudi nyumbani na kuwekeza nchini mwao, ambako uchumi unadidimia na unatakiwa uwekezaji mpya.

    Rais Mnangagwa amesema hayo kwa jamii ya wafanyabiashara wa Wazimbabwe wakati wa ziara yake ya siku moja nchini Msumbiji, na kuongeza kuwa serikali yake inajitahidi kukabiliana na vikwazo vyote vya kisheria vinavyokwamisha biashara nchini Zimbabwe.

    Naye rais Felipe Nyusi wa Msumbiji ameeleza kuunga mkono kauli ya rais Mnangagwa. Rais Felipe amewaambia wafanyabiashara hao wakipata nafasi wakaangalie fursa zilizoko nchini mwao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako