Takwimu zilizotolewa na Idara ya Hakimiliki ya Taifa ya China zinaonesha kuwa, mwaka jana hataza za uvumbuzi ziliongezeka taratibu nchini China, na wastani wa umiliki wa hataza hizo kwa wachina ulikuwa 9.6 kwa watu laki moja.
Mwaka jana maombi ya hataza za uvumbuzi yaliongezeka kwa asilimia 14.2 kuliko mwaka juzi na kufikia milioni 1.382, ambazo kati yao laki 4.2 ziliidhinishwa kuwa hataza.
Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, hataza za uvumbuzi zimefikia milioni 1.356 China bara.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |