• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema ushirikiano wa kiuchumi kati yake na Uingereza una uwezo mkubwa wa maendeleo

    (GMT+08:00) 2018-01-18 19:03:17

    Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, ushirkiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Uingereza una uwezo mkubwa wa maendeleo.

    Bw. Gao amesema, Uingereza ni mwenzi muhimu wa kiuchumi na kibiashara wa China barani Ulaya. Mwaka jana biashara kati ya pande hizo mbili iliongezeka kwa asilimia 6.2 na kufikia dola bilioni 79.03 za kimarekani. Uuzaji wa bidhaa wa China kwa Uingereza pia uliongezeka kwa asilimia 1.8 huku uagizaji kutoka Uingereza ukiongezeka kwa asilimia 19.4.

    Uwekezaji wa Uingereza nchini China ulifikia dola bilioni 1.5 za kimarekani na uwekezaji wa China usio wa kifedha nchini Uingereza ulifikia dola bilioni 1.53 za kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako