• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kushirikiana na nchi mbalimbali kupambana na ujangili na biashara harumu za wanyama pori

    (GMT+08:00) 2018-01-18 19:38:21

    China itaendelea kushirikiana na nchi za Afrika na jumuiya ya kimataifa katika kupambana na ujangili na biashara haramu za wanyama na mimea pori.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lu Kang leo amesema, China ikiwa nchi iliyosaini Mkataba wa Biashara ya Kimataifa kuhusu Viumbe vilivyo Hatarini Kutoweka, imetekeleza wajibu wake huo kwa makini na kwa muda mrefu. Ameongeza kuwa kuanzia tarehe Mosi, Januari mwaka huu, biashara zote za pembe za Ndovu na bidhaa za pembe hizo zimekuwa haramu China bara, hatua ambayo imepongezwa na nchi mbalimbali za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako