• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali kuondoa marufuku ya safari za usiku

    (GMT+08:00) 2018-01-18 20:03:48

    Serikali inatarajiwa kuondoa marufuku dhidi ya usafiri wa usiku katika muda wa wiki mbili.

    Katibu katika wizara ya uchukuzi Paul Mwangi Maringa ametanagaza kuwa marufuku dhidi ya usafiri wa usiku uliowekewa magari ya uchukuzi wa umma yataondolewa kuanzia kati kati ya mwezi ujao.

    Akifika mbele ya kamati ya bunge kuhusu uchukuzi , Mwangi hata hivyo alisema vyama vya Matatu vitalazimika kutimiza masharti fulani kabla ya kuondolewa kwa marufuku hayo. Mwangi amesema wizara hiyo imekuwa ikiandaa mazungumzo na wadau kuhusu marufuku hayo.

    Kamati hiyo ya bunge kuhusu uchukuzi ikiongozwa na mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing pia iliwahoji maafisa wa halmashauri ya kitaifa kuhusu uchukuzi na usalama barabarani NTSA , maafisa wa idara ya trafiki , na katibu katika wizara ya muundo msingi John Mosonik kuhusiana na vifo vilivyotokana na ajali za barabarani.

    Halmashauri ya NTSA ilipiga marufuku usafiri wa masafa marefu wakati wa usiku mwishoni mwa mwaka uliopita kama mkakati wa kukabiliana na ajali za barabarani zilizosababisha vifo vya watu kadhaa mwezi Disemba.

    Halmashauri hiyo imesema nyingi za ajali hizo hutokea usiku na hivyo kusababisha kupigwa marufuku kwa usafiri wa usiku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako