• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania :Kampuni zaagizwa kuchukua sukari bandarini

    (GMT+08:00) 2018-01-18 20:10:46

    Tanzania imeamrisha kuchukuliwa kwa sukari ya viwandani iliyokwama katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuviwezesha viwanda vitano vilivyoagiza visifungwe kwa kukosa malighafi .

    Hatua hiyo imefikiwa baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuishauri serikali kuruhusu sukari hiyo iliyokuwa inashikiliwa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kuchukuliwa ili kuviokoa viwanda hivyo.

    Viwanda vilivyolalamika sukari yao kuzuiwa na TRA bandarini ni Kiwanda cha Sayona cha Dar es Salaam na Mwanza, Kiwanda cha Ivory cha Iringa, Kiwanda cha Iringa Food Beverage cha Iringa na Kiwanda cha Anjari cha Tanga.

    Uamuzi wa kupewa masharti ya mikataba kwa viwanda hivyo, ulifikiwa mjini hapa jana katika kikao kilichowajumuisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Sadick Murad, Mnadhimu wa Shughuli za Serikali bungeni ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Jenista Mhagama na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.

    Majadiliano hayo pia yalimhusisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango aliyeshiriki kwa njia ya simu na baadaye kufikiwa uamuzi wa viwanda hivyo kupewa masharti ili kuviwezesha kuchukua sukari yao bandarini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako