• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea kaskazini yailaani Marekani kuitisha mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kuhusu suala la Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-01-19 08:46:08

    Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini imeilaani Marekani kuitisha mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kuhusu suala la Korea Kaskazini, na kuona hatua hiyo inalenga kuhujumu mwelekeo wa kuboreka kwa hali ya peninsula ya Korea. Msemaji wa wizara hiyo amesema hivi sasa dunia nzima inapongeza maendeleo yaliyopatikana katika kupunguza mvutano kwenye peninsula ya Korea, lakini Marekani inaenda kinyume na mwelekeo huo mzuri, na kuitisha mkutano wa nchi zilizowahi kuivamia Korea kaskazini kujadili kuongeza shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini, na kupanga kuanzisha vita mpya kwenye peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako