• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani kufanya ziara Ulaya

    (GMT+08:00) 2018-01-19 08:46:27

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson atafanya ziara nchini Uingereza, Ufaransa, Poland na Uswisi kuanzia tarehe 21 hadi 27 mwezi huu, wakati mgawanyiko kati ya Ulaya na Marekani unazidi kuwa mkubwa, baada ya Marekani kupendekeza kupitiwa upya kwa Makubaliano ya nyuklia ya Iran. Uhusiano kati ya Ulaya na Marekani umepungua tangu rais Donald Trump wa Marekani aingie madarakani, na tofauti kubwa zimejitokeza zaidi kati ya pande hizo mbili juu ya masuala mbalimbali ya kimataifa, ikiwemo Marekani kujitoa katika makubaliano ya Paris, uamuzi wa Marekani kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel na kutotambua kuwa Iran inatekeleza makubaliano ya nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako